Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria yaruhusu WFP kusambaza misaada

Syria yaruhusu WFP kusambaza misaada

Hatimaye serikali ya Syria imeruhusu shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo kusambaza vyakula vya misaada kwa watu Milioni Mbili na Nusu walionaswa katika shida kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo.

Mkurugenzi mkuu wa WFP Ertharin Cousin ameaambia waandishi wa habari mjini Geneva leo kuwa wamepata kibali hicho na wamepatiwa orodha ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya kushirikiana nayo.

(SAUTI Cousin)

Tayari Bi. Cousin ametembelea kambi ya wakimbizi wa Syria ya Kilis iliyoko kwenye mpaka wa Syria na Uturuki.