Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya raia akiwemo mbunge huko Iraq

UM walaani mauaji ya raia akiwemo mbunge huko Iraq

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Martin Kobler ameshutumu vikali mauaji ya mbunge Ifan Al-Issawi nchini Iraq yaliyotokana na shambulio la kigaidi wakati wa maandamano huko Fallujah ambapo pia watu kadhaa waliuawa na wengine walijeruhiwa.

Kobler ambaye anaongoza ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi nchini Iraq UNAMI amesema ni muhimu kuhakikisha maandamano yanakuwa salama na yanalindwa dhidi ya magaidi.

Pamoja na kutaka vikundi vyote vya kisiasa nchini Iraq kufichua majaribio yoyote ya kuleta vurugu na kujizuia kufanya mashambulizi, Bwana Kobler ametuma rambi rambi kwa familia za marehemu na kuwatakia majeruhi uponaji wa haraka.