Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya waliovuka ghuba ya Aden yavunja rekodi

Idadi ya waliovuka ghuba ya Aden yavunja rekodi

Takriban wakimbizi na wahamiaji 107,500 walifanya safari zilizo hatari kutoka pembe ya Afrika kwenda nchini Yemen mwaka 2012 ikiwa ndiyo idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na wahamiji kuwahi kuandikishwa tangu mwaka 2006 wakati shirika la kuhudumia wakimbzi la Umoja wa Mataifa UNHCR lilipoanzisha ukusanyaji wa takwimu hizo.

UNHCR inasema kuwa wanane kati watu kumi waliowasili walikuwa ni raia wa Ethiopia huku waliosalia wakiwa ni raia wa Somalia. Wahamiaji wengu hutumia taifa la Yemen kama kivukio kwenda mataifa ya ghuba.

Ikiwa tayari inakabiliwa na chamgamoto za kiuchumi na usalama, Yemen imekuwa ikiwapokea watu wengi kutoka pembe ya Afrika wanaokimbia kutafuta usalama na riziki. Hadi sasa Yemen imetoa hifadhi ya hadi wakimbizi zaidi ya Laki Mbili wengi wao wakiwa ni raia wa Somalia.