Jeshi la Afrika kwenda Mali punde

14 Januari 2013

Baraza la usalama hii leo lilikuwa na kikao  kuhusu hali ilivyo huko Mali ambapo Balozi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gerard Araud amesema wajumbe wote wa baraza wameunga mkono hatua za kijeshi za Ufaransa kwa ridhaa ya Mali.

Bwana Araud amewaambia waandishi wa habari kuwa tayari nchi zingine ikiwemo Marekani, Canada na Uingereza zimeonyesha nia ya kutoa msaada wa vifaa na kwamba jeshi la Umoja wa Afrika litakwenda Bamako, Mali siku chache zijazo likiongozwa na Kamanda kutoka Nigeria.

Amesisitiza kuwa kile kinachotekelezwa ni kwa mujibu wa azimio 2085 la Baraza la Usalama na kwamba kile kinachofanyika kinalenga kuwezesha mchakato wa kisiasa na amani ya kudumu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter