Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoibuka kiuchumi zapongezwa kwa kumulikia afya

Nchi zinazoibuka kiuchumi zapongezwa kwa kumulikia afya

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na HIV na Ukimwi, UNAIDS Michel Sidibé amepongeza hatua za nchi zinazoibukia kiuchumi duniani ambazo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, BRICS ya kuazimia kushirikiana kuboresha sekta ya afya duniani.

Mathalani amegusia dhima ya kipekee ya nchi hizo kutumia uzoefu wao wa kupambana na Ukimwi kama kichocheo cha ubunifu, utafiti na maendeleo ya tiba kwa nchi zinazoendelea. Bwana Sidibe alisema hayo mwishoni mwa mkutano wa mawaziri wa afya wa nchi hizo uliomalizika nchini India. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)