Tusipuuze ukiukwaji haki za binadamu Korea Kaskazini: Pillay

14 Januari 2013

Kamishna mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua kutatua suala la haki za binadamu nchini Korea Kaskazini akisema kuwa wakati umewadia wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu uhalifu ambao umekuwa ukiendelea nchini humo kwa miaka mingi.

Pillay amesema kuwa kulikuwa na matumani ya mabadiliko kwenye masuala ya haki za binadamu baada ya kufanyika mabadiliko ya uongozi lakini mwaka mmoja baada ya Raias Kim Jong Un kushika usukani hakuna dalili zozote za mabadiliko.

Amesema mipango ya nyuklia ya Korea Kaskazini haiwezi kuruhusiwa kugubika suala la haki za binadamu nchini humo ambalo kwa njia moja au nyingine limewaathiri watu wengi.

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Halikadhalika Bin Pillay ametaka kuchunguzwa kwa hatma ya raia wa Korea Kusini na wale wa Japan waliotekwa nyara miaka kadhaa iliyopita na Korea Kaskazini.