Hali ya wakimbizi CAR inatutia wasiwasi: UNHCR

11 Januari 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linataka kuwafikia wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati bila masharti yoyote kwa kuwa lina wasiwasi kuwa hali zao zitakuwa ni mbaya.

Msemaji wa UNHCR Adrian Edwrds akizungumza mjini Geneva leo amesema maelfu ya watu wamekimbia makazi  yao kutokana na mapigano kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo wakati huu ambapo nchi hiyo inahifadhi pia wakimbizi kutoka nchi nyingine. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa George Njogopa.

(SAUTI YA ADRIAN)

"Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya ustawi wa jumla wa raia, wengi wao wakiishi mazingira magumu na kwenye makazi ya mbali. Vile vile wakimbizi kutoka nchi kama vile Sudan Kusini, Chad na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud