Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yataka kusitishwa mapigano ya kikabila kwenye eneo la Jebel Amer

UNAMID yataka kusitishwa mapigano ya kikabila kwenye eneo la Jebel Amer

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za Afrika kwenye jimbo la Darfur UNAMID unasema kuwa umetiwa wasi wasi na mapigano kati ya kabila za Hussein na Abbala katika eneo la Jebel Amer karibu na Kabkabiya Darfur kaskazini. Mapigano hayo yanayoripotiwa kuanza tarehe tano mwezi Januari mwaka huu yamesabisha mauaji ya watu kadha , uporaji , kuchomwa kwa vijiji na kukimbia kwa raia wakielekea miji ya Kabkabiya, Saraf Omra na Al Sereif .

Mjumbe kwenye ujumbe wa UNAMID Aichatou Mindaoudou tayari amefanya mazungumzo kuhusu kisa hicho na gavana wa jimbo la Darfur Kaskazini bwana Othman Kibir. Ujumbe wa UNAMID uliendesha usafirishaji kwa njia za ndege ambapo uliwahamisha watu 26 kutoka miji ya Al Serif na Kabkabiya kwenda El Fasher.