Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya Mali yatishia usalama wa kikanda na dunia: UM

Hali ya Mali yatishia usalama wa kikanda na dunia: UM

Wajumbe wa Baraza la usalama waliokutana katika kikao cha dharura jioni ya leo kuhusu Mali wameeleza kusikitishwa kwao na ripoti ya kwamba vikundi vya kigaidi na vyenye msimamo mkali kaskazini mwa nchi hiyo vinaendelea na mashambulizi, wakigusia zaidi taarifa za kutekwa kwa mji wa Konna.

Rais wa Baraza hilo Balozi Masood Khan amewaambia waandishi wa habari baada ya kikao hicho kuwa wajumbe hao wamesema kuzorota kwa hali ya usalma kunatishia siyo tu utulivu na ustawi wa Mali bali pia ni kitisho kwa amani na usalama duniani.

Kwa mantiki hiyo wajumbe hao wamerejelea maazimio kadhaa dhidi ya Mali ikiwemo namba 2056, 2071 na 2085 na kutoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kusaidia kumaliza mzozo wa Mali ikiwemo kutoa usaidizi kwa vikosi vya ulinzi.

(SAUTI YA KHAN)

“Wajumbe wa Baraza la usalama wanaeleza azma yao ya kufuatilia utekelezaji wa kina wa maazimio yake dhidi ya Mali hususan azimio namba 2085 kwa mapana yake. Kwa mantiki hiyo wanataka kupelekwa haraka kwa kikosi cha Afrika chenye usaidizi wa kimataifa kwa ajili ya kusaidia Mali-AFISMA.”

Gérard Araud ni Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa na ndiye ambaye nchi yake ilipendekeza kuitishwa kwa kikao hicho cha dharura hii leo jioni.

 (SAUTI YA Araud)