Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zebaki tishio la afya na mazingira: UNEP

Zebaki tishio la afya na mazingira: UNEP

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP limesema kadri siku zinavyosonga, zebaki inazidi kutishia afya ya binadamu na mazingira katika nchi zinazoendelea kutokana na ongezeko la uchafuzi wa mazingira utokanao na madini hayo.

UNEP imesema metali hiyo yenye sumu hutumiwa na wachimbaji wadogo katika shughuli zao na pia katika uchomaji wa makaa ya mawe kwa ajili ya kuzalisha umeme huko Afrika, Asia na Amerika ya Kusini. Monica Morara na taarifa zaidi.

(SAUTI YA MONICA MORARA)