Baada ya tetemeko, Haiti inajikwamua:UM

Baada ya tetemeko, Haiti inajikwamua:UM

Miaka mitatu tangu tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti, Umoja wa Mataifa umesema jitihada za kusadia nchi hiyo kurejea katika hali yake ya kawaida zimetia matumaini ikiwemo ujenzi wa shule, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

Hiyo ni kauli ya Afisa Mtendaji Mkuu wa wakfu ya Umoja wa Mataifa Kaithy Calvin aliyoitoa alipozungumza na waandishi wa habari kabla ya kumbukumbu ya tetemeko hilo siku ya Jumamosi. Tetemeko hilo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu Laki Tatu na wengine zaidi ya Milioni Moja bila makazi.

Bi. Calvin amesema mafanikio yaliyopatikana hadi sasa yanatokana na ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa, Marekani na serikali ya Haiti na wananchi ambao wanashiriki kujenga upya nchi yao.

(SAUTI YA KATHY)

"Asilimia 80 ya kifusi kilichotokana na tetemeko hilo tayari kimeondolewa kwa ushirikiano kati ya serikali na wananchi wa Haiti na washirika wao kama vile Umoja wa Mataifa. Tatizo la makazi limepatiwa suluhu ambapo familia Laki Moja na Elfu Hamsini nane zilizopoteza makazi zimepatiwa nyumba. Takribani watoto milioni Tatuu wenye umri wa chini ya miaka 10 wamepatiwa chanjo dhidi ya surua, polio na rubella. Zaidi ya nafasi Laki Nne na Elfu Sabini za ajira za muda zimepatiakan ambapo asilimia 40 ya wafanyakazi hao ni wanawake.”

Naye Afisa habari kutoka Idara ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa Andre- Michel Essoungou amesema kwa sasa wanaweza kuendelea na jukumu lao la kusaidia mchakato wa siasa kwa kuwa kwa miaka mitatu walinzi wa amani walihusika zaidi na utoaji wa misaada ya kibinadamu baada ya tetemeko la ardhi.