Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wakutana Seoul kujadili matatizo yanayokumba eneo la Asia

Vijana wakutana Seoul kujadili matatizo yanayokumba eneo la Asia

Nafasi za ajira, kutokuwepo kwa usawa, mazingira, usawa wa kijinsia, amani na usalama huko Kaskazini-mashariki mwa Asia ni miongoni mwa masuala kuu ambayo vijana wa eneo hilo wanataka yazingatiwe katika ajenda ya baadaye ya maendeleo. Washirikishi vijana kutoka nchi kama vile China, Japan na Mongolia wameafikia makubaliano kuhusu maendeleo ya dunia yenye kauli mbiu “Ulimwengu tunaohitaji”.

Makubaliano hayo yalifikiwa mjini Seoul, Korea Kusini kwenye mkutano mkuu wa vijana ikiwa ni sehemu ya majadiliano yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa kabla ya mwaka mwaka 2015 ulio ukomo wa kipimo cha malengo ya maendeleo ya milenia. Vijana katika mkutano huo walizungumza wazi ambapo wanataka watoa maamuzi wahakikishe kuwepo kwa elimu na ulimwengu ulio wenye usawa na pia ulio salama na amani.