Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Canada kufanya mazungumzo ya viongozi wa kitamaduni

Serikali ya Canada kufanya mazungumzo ya viongozi wa kitamaduni

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya jamii za kiasili James Anaya ametoa wito kwa serikali ya Canada kufanya mazungumzo na viongozi wa kitamaduni nchini humo kufuatia kushuhudiwa kwa maandamano hivi majuzi.

Mjumbe huyo amesema amefurahishwa na ripoti kwamba waziri mkuu wa Canada Steven Harper amekubali kukutana na viongozi hao kuzungumzia masuala yakiwemo maendeleo ya kiuchumi. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)