Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa majumbani Tanzania hawajitambui: ILO

Wafanyakazi wa majumbani Tanzania hawajitambui: ILO

Ofisi ya ILO nchini Tanzania imesema bado kuna changamoto kubwa ya kuweza kuwakomboa wafanyakazi wa majumbani dhidi ya matatizo yanayowakabili licha ya kwamba sheria za kazi zinawatambua.

Mratibu wa mpango wa misaada ya maendeleo katika ofisi ya ILO nchini Tanzania, Anne-Marie Kiaga ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa changamoto hizo ni za pande tatu akitaja usimamizi wa sheria, waajiriwa wenyewe pamoja na waajiri.

(SAUTI  YA ANNE-MARIE)

Bi. Kiaga amesema hata wakati huu ambapo ILO kwa kushirikiana na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali inaendesha utafiti wa kina kufahamu idadi halisi ya wafanyakazi wa majumbani nchini Tanzania kuna changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo kujitambua na hivyo kinachofanyika ni kuelimisha umma.

(SAUTI – ANNE-MARIE)