Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bahrain iwaachie mara moja watetezi wa haki za binadamu: UM

Bahrain iwaachie mara moja watetezi wa haki za binadamu: UM

Ofisi ya Kamishna wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, imetaka kuachiwa mara moja kwa raia 13 wa nchi hiyo waliohukumiwa kifungo jela kwa kufanya maandamano dhidi ya serikali ya nchi hiyo.

Ofisi hiyo imeeleza kusikitishwa na kifungo cha wanaharakati hao baada ya miaka miwili ya kesi licha ya matokeo ya tume huru ya uchunguzi ya Bahrain na wito wa jumuiya ya kimataifa kuhusu taratibu za kimahakama na madai ya watu hao kuteswa. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI GEORGE)