Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uswisi yatunisha mfuko wa IOM

Uswisi yatunisha mfuko wa IOM

Shirika la kimataifa la uhamaiaji IOM pamoja la lile la maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC) yametia sahihi makubaliano ya mradi utakaowasaidia raia wa Chad waliorejea nyumbani kutoka Libya ambao kwa sasa wanaishi kwenye mikoa mitatu ya kaskazini iliyo jirani na mpaka wa Libya, Niger na Sudan.

Msaada huo wa dola Milioni 2.9 kutoka Uswisi utasaidia shughuli za kijamii kwa raia wa Chad.

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Inakadiwa kuwa watu 125,000 waliorejea nyumbani watanufaika na mpango huu ambapo Bwana Jumbe amezungumzia changamoto zinazowakabili raia hao.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)