Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kurejea wakimbizi ni dalili nzuri: Balozi Mahiga

Kurejea wakimbizi ni dalili nzuri: Balozi Mahiga

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Somalia, Balozi Augustine Mahiga ametolea ufafanuzi kitendo cha kurejea kwa wakimbizi wa Somalia nchini mwao ambapo amesema wakimbizi hao wanarejea kwa hiari yao wenyewe kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama nchini mwao.

Balozi Mahiga amesema hayo katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA-1)

Hata hivyo Balozi Mahiga amesema ujio huo ni changamoto kwa serikali ya Somalia kwa kuwa haikuwa imejiandaa na hivyo Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kusaidia serikali ya Somalia kuhakikisha inasaidia wakimbizi hao kujumuika tena upya ndani ya nchi yao.

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA-2)