Skip to main content

Niko tayari kwenda Guinea-Bissau: Ramos-Horta

Niko tayari kwenda Guinea-Bissau: Ramos-Horta

Mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Guinea-Bissau Jose Ramos Horta amesema yuko tayari kwenda nchini humo kutekeleza majukumu ya kuwezesha kurejea kwa amani na utulivu.

Akizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Ramos- Horta amesema anafahamu fika hali halisi ya Guinea-Bisssau kwa kuwa alishakwenda nchini humo, mara ya kwanza akiwa waziri wa mambo ya nje wa Timor- Letse na mara ya pili pia akiwa mjumbe maalumu wa nchi zinazozungumza lugha ya kireno.

(SAUTI HORTA)

Bwana Ramos-Horta anakuwa Mkuu wa ofisi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini humo na anachuka nafasi iliyoachwa wazi na Joseph Mutaboba kutoka Rwanda.