Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO kuzindua ripoti kuhusu wafanyakazi wa majumbani

ILO kuzindua ripoti kuhusu wafanyakazi wa majumbani

Shirika la kazi duniani, ILO wiki ijayo itazindua ripoti mpya kuhusu hali za wafanyakazi wa majumbani duniani kote.

Ripoti hiyo mpya inajaribu kugusia ukubwa wa sekta hiyo, mazingira ya kazi na mawanda ya ulinzi wa kisheria kwa wafanyakazi hao wa majumbani.

Mathalani inajumuisha takwimu za dunia na za kikanda na inalenga kusaidia jitihada za serikali, waajiri na wafanyakazi wenyewe za kupata haki ya kijamii na kazi yenye staha kwa watumishi wa majumbani duniani kote.