Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchoraji unavyopanua uelewa wa watoto

Uchoraji unavyopanua uelewa wa watoto

Nchi nyingi barani afrika zinalalamikiwa kutokana na kutoweka mazingira mazuri ya kuendelea vipaji vinavyochomoza kwa watoto. Hali hiyo imefanya ndoto za vijana wengi kuishia hewani kutokana na kukosa daraja la kuwaendeleza. Lakini nchini Tanzania nuru imeanza kuchomoza kidogo baada ya kueanzishwa darasa maalumu kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kisanaa.

Sanaa hii inaelezwa kuwa kichocheo kikubwa katika kupanua uelewa wa mtoto. Hii ni kwa sababu mtoto anapoamua kuchora kitu, lazima afikirie anataka kuchora nini na lazima kiwe na uwiano mathalani ya kiukubwa na hata rangi anazotumia. Basi katika makala yetu, mwenzetu George Njogopa anaangalia uanzishwaji wa darasa hilo pamoja na matarajio katika siku za usoni, karibu kuungana naye.

(PKG YA GEORGE NJOGOPA)