Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tisa wawania wadhifa mkuu WTO

Tisa wawania wadhifa mkuu WTO

Jumla ya watu Tisa waliwasilisha majina yao kuwania nafasi ya Ukurenzi Mkuu wa Shirika la biashara duniani, WTO ambapo mkurugenzi Mkuu wa sasa Pascal Lamy kipindi chake kinakoma tarehe 31 mwezi Agosti mwaka huu.

Taarifa ya WTO inataja nchi wanazotoka watu hao kuwa ni Brazili, Jamhuri ya Korea, Mexico, Jordan, Costa Rica, New Zeland, Ghana, Indonesia na Kenya.

Anayewakilisha Kenya katika kinyang’anyiro hicho ni Balozi Amina Mohammed ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP.

Uwasilishaji majina ulikoma tarehe 31 mwezi uliopita ambapo baraza kuu la shirika hilo litakutana tarehe 29 mwezi huu kwa wagombea kujitambulisha.

Uchaguzi unapaswa kuwa umekamilika si zaidi ya tarehe 31 mwezi Mei mwaka huu.