Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wachezaji wa NBA watoa chanjo za Polio Kenya

Wachezaji wa NBA watoa chanjo za Polio Kenya

Kundi la wachezaji mashuhuri wa ligi ya mpira wa kikapu NBA kutoka Marekani wameitembelea Kenya katika shughuli ya kupambana na ugonjwa wa kupooza.

Wakiwa kwenye wilaya ya Turkana wachezaji hao wakiwemo Luc Mbah a Moute, Nick Collison and Dikembe Mutombo waliungana na kampeni ya kutoa chanjo ya nyumba hadi nyumba ya kuwachanja watoto wa eneo hilo dhidi ya ugonjwa wa kupooza.

Bwana Collison anasema kuwa aliweza kuwapatia chanjo watoto kadha jambo lililoonekana kumtia moyo akiongeza kuwa sasa maisha ya watoto hao yameokolewa.

Wachezaji hao pia waliweka alama ya nyumba ambako watoto walichanjwa kwa kuwa chanjo hiyo hurudiwa.

Ili kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa polio nchini Kenya , shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa linawasaidia kuishi maisha mazuri na pia katika kuwakinga watoto wengine barani Afrika na nje.