Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahitimisha urejeshaji wakimbizi wa Liberia

UNHCR yahitimisha urejeshaji wakimbizi wa Liberia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekamilisha mpango wake wa kurejesha nyumbani kwa hiari wakimbizi 155,000 wa Liberia waliokuwa wanaishi uhamishoni kwa miaka 23 baada ya kuanza kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao.

Kundi la mwisho la wakimbizi 724 waliondoka kutoka Guinea na hivyo kukamilisha mpango huo ulioanza mwaka 2004, mwaka mmoja baada ya amani kurejea nchini mwao. UNHCR imesema kwa mantiki hiyo mpango wa kuwarejesha makwao kwa hiari wakimbizi wa Liberia umemalizika. Tupate taarifa zaidi.