Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo CAR, watoto watumikishwa jeshini: UNICEF

Mzozo CAR, watoto watumikishwa jeshini: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetaka kusitishwa mara moja kwa vitendo vinavyofanywa na vikundi vyenye silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR vya kuandikisha watoto kwenye majeshi.

UNICEF imetaka pande zote katika mzozo unaoendelea nchini humo kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote hatari ikiwemo kuhusishwa na mgogoro huo.

Tamko la UNICEF linafuatia ripoti za uhakika ya kwamba vikundi vya waasi na wanamgambo wanaounga mkono serikali wanatumikisha watoto jeshini ili washiriki katika mapigano yanayoendelea. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)