Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utalii wa mazingira hutokomeza umaskini: UM

Utalii wa mazingira hutokomeza umaskini: UM

Shirika la Umoja wa Mataifa la utalii, limesema kupitishwa kwa azimio linalotambua utalii wa viumbe na mazingira kama moja ya njia ya kupambana na umaskini na kulinda mazingira ni kitendo cha kupongezwa na kimefanyika wakati muafaka.

Kwa mantiki hiyo shirika hilo limetaka nchi wanachama kubuni sera zitakazosaidia kuinua utalii wa mazingira ambao pia husaidia kutokomeza njaa. Monica Morara na taarifa kamili

(SAUTI YA MONICA MORARA)