Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yasaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii DRC

MONUSCO yasaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii DRC

Kikundi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kimekamilisha ukarabati wa barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa 600 kwenye ukanda ulioathiriwa na vita Mashariki mwa nchi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha amani na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mkuu wa ofisi ya MONUSCO jimbo la Kivu Kusini Aliou Sene amesema barabara hizo ziliharibiwa na mvau kubwa na hivyo kukata mawasiliano baina ya miji ya Bunyakiri na Hombo huko Kivu Kusini.

Sene amesema pamoja na ukarabati wa barabara wamekarabati daraja la Bunyakiri lililoharibiwa na mvua kubwa na kusababisha watu kushindwa kusafiri kati kati ya vitongoji vilivyo pande tofauti za daraja hilo.

"MONUSCO iko hapa na MONUSCO itaendelea kusaidia wananchi wa Bunyakiri na Hombo. Itasaidia vijana wa Bunyakiri na Hombo siyo tu kwa shughuli za michezo na utamaduni bali pia kwenye shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.”

Mmoja wa vijana wanaoishi eneo hilo amesema kabla ya ukarabati wa barabara hizo hali ilikuwa ni mbaya.

(SAUTI-KISWAHILI)