Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado tuna wasiwasi mkubwa na hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati: UM

Bado tuna wasiwasi mkubwa na hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati: UM

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali ilivyo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na unaendelea kufanya mawasiliano na mwakilishi maaluma wa Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa nchini humo Margreth Voght.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo kuwa wakati wanaendelea na mawasiliano hayo umoja wa mataifa unarejelea azimio la Baraza la Usalama la tarehe 27 mwezi uliopita.

“Tunasisitiza azimio la baraza la usalama la terehe 27 mwezi uliopita linalotaka pande zote kujizuia kufanya vitendo vyote vya ghasia dhidi ya raia na kuheshimu haki za binadamu na kutafuta suluhu kwa njia ya amnai. Tunataka serikali na waasi kujikita katika mashauriano yatakayo epusha mzozo na kuwezesha suluhisho la amani na kuheshimuwa pia makubaliano ya kina ya Brazaville.”

Halikadhalika amesema kwa nia ya kujihadhari wafanyakazi wa kimataifa wote wamehamishwa kwa muda nchini humo wakati huu ambapo mashaurino ya kuleta amani yakiendelea.