Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kemikali ya sumu au Aseniki iliyo kwenye maji yaweza kusababisha kansa

Kemikali ya sumu au Aseniki iliyo kwenye maji yaweza kusababisha kansa

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO, inasema uwepo wa kemikali ya sumu, aseniki katika maji ya kunywa na chakula kwa muda mrefu unaweza kusababisha saratani na vidonda vya ngozi.

 WHO inasema aseniki imekuwa ikihusishwa na kuathiri vibaya ukuaji wa binadamu, ugonjwa wa moyo, uharibifu wa mfumo wa mishipa ya fahamu na ugonjwa wa kisukari. Ripoti hii mpya inamulika hatari itokanayo na maji yenye aseniki ambayo hutumika kwa kunywa, kupikia vyakula na umwagiliaji wa mazao ya chakula.

WHO inasema tishio kubwa zaidi kwa afya ya umma inasababishwa na maji yaliyokumbwa na aseniki chini ya ardhi ambako kemikali hiyo hupatikana kwa kiwango kikubwa hususan kwenye nchi za Argentina, Bangladesh, Chile, China, India, Mexico na Marekani.

Miongoni mwa vyakula vinavyoathiriwa na kemikali hiyo ni samaki, samakigamba, nyama, kuku, maziwa na nafaka.