Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumesikitishwa na vifo huko Cote d’Ivoire:UNOCI

Tumesikitishwa na vifo huko Cote d’Ivoire:UNOCI

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Côte d'Ivoire Bert Koenders ameelezea masikitiko yako kufuatia vifo vya watu 60 vilivyotokea saa chache baada ya kumalizika kwa mkesha wa mwaka mpya kwenye mji mkubwa zaidi nchini humo, Abidjan.

Amesema vifo na majeruhi vilivyosababishwa na msongamano kwenye uwanja ambako sherehe za mwaka mpya zilikuwa zinafanyika vimesababisha majonzi kwa raia wa nchi waliokuwa wakisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2013 uliobeba matumaini makubwa ya ujenzi wa amani, maridhiano na kujikwamua kiuchumi na kisiasa kwa wananchi wote wa Cote D’Ivoire.

Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo, UNOCI ambayo Koenders anaiongoza imemkariri akisema kuwa mara baada ya kupata taarifa za mkasa huo, ofisi hiyo ilituma jopo la wahudumu wa dharura pamoja na kutangaza utayari wa kusaidia wahanga na uchunguzi wa tukio hilo.

Idadi kubwa ya waliodhurika na msongamano huo ni wanawake na watoto