Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Jose Ramos-Horta kuwa mjumbe wake GUINEA –BISSAU

Ban amteua Jose Ramos-Horta kuwa mjumbe wake GUINEA –BISSAU

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Rais wa zamani wa Timor-Letse José Ramos-Horta kuwa mwakilishi wake maalumu nchini Guinea Bissau.Kwa wadhifa huo pia, Ramos-Horta anakuwa Mkuu wa ofisi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Joseph Mutaboba kutoka Rwanda ambapo imeelezwa kuwa Ramos-Horta kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa alisaidia kufanikisha chaguzi za Rais na wabunge nchini Timor Letse.