Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wawili wa Jordan waliokuwa wametekwa sasa huru: UNAMID

Walinda amani wawili wa Jordan waliokuwa wametekwa sasa huru: UNAMID

Walinda amani wawili wa Jordan waliotekwa wakati wakihudumu kwenye kikundi cha pamoja cha kulinda amani Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID wameachiwa huru baada ya kuwa matekani kwa siku 136.

Msemaji wa UNAMID, Aicha Elbasri amesema kwa sasa wako salama na wanaelekea mji mkuu wa Sudan, Khartoum na baadaye watakwenda Jordan baada ya kuachiwa huru huko walikokuwa wanashikiliwa eneo Zanglei, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kati.

Walinda amani hao walipotea tarehe 20 mwezi Agosti mwakajana kwenye mji wa Kebkabiya, takribani kilometa 140 magharibi mwa mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, El Fasher ambapo Umoja wa Mataifa umeonya kuongezeka kwa ukosefu wa usalama hivi karibuni.