Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matukio ya mwaka 2012

Matukio ya mwaka 2012

Hatimaye mwaka 2012 umefikia ukingoni. Kwa Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu, Ban Ki Moon alieleza kuwa ulikuwa wa mtikisiko, kuanzia mabadiliko ya tabia nchi, mapigano nchini Syria na mzozo Mashariki ya Kati, mgogoro Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, mapigano huko Mali, majanga ya asili ikiwemo vimbunga, mafuriko, njaa yote alisema yaliuweka Umoja wa Mataifa majaribuni! Lakini chombo hicho kilijitahidi kuzingatia misingi ya kuanzishwa kwake. Usimamizi wa amani, ulinzi na usalama. Assumpta Massoi anaangalia mwaka 2012 ulivyokuwa katika makala haya.