Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa maji waleta nuru kambi ya Dadaab

Mradi wa maji waleta nuru kambi ya Dadaab

Kambi ya Dadaab iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya inahifadhi wakimbizi kutoka Somalia. Kambi hii inaelezwa kuwa ni kubwa kuliko kambi zote za wakimbizi duniani ikiwa inahifadhi wakimbizi zaidi ya Laki Nne na Nusu. Uhaba wa maji umekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo. Lakini nuru imechomoza na kubadili maisha ya familia za kifugaji. Ni nuru gani hiyo? Ungana na Assumpta Massoi kwa ripoti kamili:

Soundbite 1: Play then hold under

ASSUMPTA: Miaka kadhaa sasa imepita tangu mvua inyeshe kwenye kambi hii ya Dadaab kaskazini-mashariki mwa Kenya ambako Fatima Suthi, mama mwenye umri wa miaka 51 anaishi na familia yake. Fatima amekuwa akihangaika kuishi kwenye eneo hilo kame ambalo maji ni bidhaa adimu.

Ukame umesababisha kufa kwa mifugo yake yote na kumlazimuu yeye kama ilivyo kwa familia zingine za wafugaji kubadili mfumo wa maisha ili waweze kuishi. Fatima na wanae walijihifadhi kwenye kibanda kidogo, wakati ambapo hali ya hewa ni mbaya, majani ni machache na hivyo basi ili kujikinga na jua, familia yake ikatundika makaratasi ya nailoni juu ya mti ili kujikinga na jua kali la mchana.

Soundbite: Water Play hold under……then Cue back to back Fatima

Kutokana na mazingira hayo magumu, mradi wa maji unaoendeshwa na shirika la kuhudumia watoto, UNICEF katika eneo lao ukawa ndio mkombozi na kuleta matumaini.

SOUNDBITE (Amharic) Fatima Suthi,

"Bila maji hakuna maisha. Sasa watoto wangu wa kike wanaweza kwenda shule. Kabla ya hapo walitumia muda mwingi kutafuta maji. Mradi huu umebadili maiha yangu.”

ASSUMPTA: UNICEF iliweka kibanda cha kuuza maji kwenye eneo la shule. Wakazi wanalipa fedha kidogo tu kupata maji hayo ambapo fedha inayopatikana inatumika kununua petroli ya kuendesha jenereta ya mradi huo. Halikadhalika kulipa mishahara ya walimu, mlinzi na pia kusaidia malipo ya ada ya shule kwa watoto wasio na uwezo.

SOUNDBITE (Somali) Mohamued Abdi Osman, School Chairman:

"Awali maisha hapa yalikuwa magumu sana. Hivi sasa familia zinapeleka watoto wao shule kwa sabab maji yanapatikana hapa. Baada ya mifugo mingi kufa kutokana na ukame, matumaini ya familia za wafugaji wanaohamahama yalibakia kwa watoto wao kupata elimuu. Mradi wa maji uko hapa shule na unafanya hilo liwezekane.”

Kwa sasa jamii iko na afya, furaha na imejiandaa vyema kukabiliana na ukame. Na kwa watoto, wanaendelea kupata elimu, ikiwa ni mara ya kwanza katika maisha yao, faida ambayo itadumu vizazi na vizazi.

Naam ilikuwa ni ripoti yake Assumpta Massoi.