Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yamkana mtu aliyedai kuwakilisha shirika hilo Ureno na Ulaya Kusini

UNDP yamkana mtu aliyedai kuwakilisha shirika hilo Ureno na Ulaya Kusini

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP limesema halimtambui Artur Baptista da Silva, mtu ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa ni msemaji wake wa masuala ya Uchumi kwa Ureno na Ulaya Kusini.

Taarifa ya UNDP imesema Da Silva siyo mtumishi wala hajawahi kuajiriwa na shirika hilo na kwamba maoni yoyote aliyotoa ni ya kwake mwenyewe na wala siyo ya shirika hilo.