Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko Pakistani: Maelfu bado wahaha bila makazi ya kudumu

Mafuriko Pakistani: Maelfu bado wahaha bila makazi ya kudumu

Maelfu ya wananchi wa Pakistan ambao waliathiriwa na mafuriko ya mwezi wa Septemba bado hawajarejea kwenye maeneo yao ya awali.

Mashirika ya kutoa misaada yamesema kuwa idadi kubwa waathirika hao bado wanaendelea kusalia kwenye makambi na wengine kwenye mabanda kufuatia maeneo yao kuharibiwa vibaya na mafuriko. Kiasi cha watu milioni 4.8 wanaripotiwa kuathiriwa na mafuriko hayo yaliyoharibu pia zaidi ya nyumba 630,000. George Njogopa na taarifa zaidi:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)