Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia yatumika kurahisisha huduma kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

Teknolojia yatumika kurahisisha huduma kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

Teknolojia mpya na ya kisasa ndiyo iliyotajwa kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuyafikia mahitaji ya wakimbizi wengi wa Sudan Kusin.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR, linatumia teknolojia mbalimbali ikiwemo mifumo ya satelite pamoja na mifumo mengine ya kiteknolojia kuwafikishia ujumbe wakimbizi hao.

Pia shirika hilo linatumia teknolojia hiyo kutoa misaada ya aina mbalimbali pamoja ile ya ulinzi kwa wale walioko kwenye maeneo hatarishi.

Kwa hivi sasa UNHCR inaendesha zoezi la kusajili wakimbizi kwa kutumia mfumo mpya ambao unawezesha kukusanya taarifa za wakimbizi hao katika hali ya uhakika kabisa.