Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yakamilisha utoaji wa misaada Mashariki mwa DRC

IOM yakamilisha utoaji wa misaada Mashariki mwa DRC

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha oparesheni ya siku nne ya kuwagawia misaada isiyo chakula watu 6,500 waliohama makwao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kati ya misaada iliyosambazwa kwenye eneo la Bulengo ni pamoja na matandiko ya kulalia, mablanketi, sabuni, vyombo vya jikoni na pia nguo. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)