UNHCR yasaidia waathirika wa vitendo vya Ubakaji huko Goma

28 Disemba 2012

Kliniki ya muda iliyoanzishwa kwenye kambi ya Mugunga mjini Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC kwa ajili ya kusaidia wanawake waliokumbwa na visa vya ubakaji imeripotiwa kuwa mkombozi kwa makumi ya wanawake na wasichana waliokumbwa na mkasa huo.

Afisa wa tiba katika kituo hicho Barubeta Maombi amesema msaada wanaotoa ni wa vipimo na kama hali ikiwa ni mbaya zaidi mhusika anaelekezwa kwenda kituo cha juu zaidi cha afya.

(SAUTI BARUBETA)- French

"Kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa ngono, ndani ya saa 72 tunawapatia kifurushi kinachoitwa PEP kwa ajili ya vipimo. Kwa wasichana na wanawake, kama kuna matatizo makubwa zaidi tunawaelekeza waende hospitali ya Keshero.”

Mmoja wa wahanga wa vitendo vya ukatili wa ngono, ni mtoto mwenye umri wa miaka 17 ambaye jina lake limehifadhiwa kwa usalama na alieleza kile ambacho kilimkuta.

(SAUTI YA FLO) Swahili

"Nilikuwa nalima shambani. Walikuja, wakanitishia na bunduki zao. Waliniambia kuwa iwapo hutaturuhusu tukubake tunakuua. Na hivyo waliniangusha,wakanibaka na kuniacha.”

Kwa mujibu wa kliniki hiyo ya UNHCR kwa sasa binti huyo ni mjamzito na anatarajia kujifungua baada ya kupatiwa ushauri nasaha.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter