Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kupiga vita ukeketaji wa wanawake

Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kupiga vita ukeketaji wa wanawake

Makala yetu wiki hii ambayo pia ni ya mwisho kwa mwaka huu wa 2012 inaangazia Azimio la aina yake lililopitishwa na Umoja wa Mataifa la kupiga vita ukeketaji wa wanawake.

Harakati za kupiga vita ukeketaji wa wanawake, wasichana na watoto wa kike zinazidi kuzaa matunda. Na hatua ya hivi karibuni zaidi ni ile ya Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 20 mwezi huu kupitisha azimio lililoitwa la kihistoria dhidi ya kitendo hicho ambacho kinaelezwa kuwa na madhara makubwa ya kiafya kwa wanawake na watoto wa kike. Shirika la afya duniani, WHO linasema kuwa zaidi ya wanawake, wasichana na watoto wa kike Milioni 140 duniani kote wamekumbwa na kitendo hicho. Maeneo ambako FGM hutekelezwa ni pamoja na Afrika Kaskazini, Mashariki, Magharibi, barani Asia na Mashariki ya Kati. Assumpta Massoi alifuatilia upitishwaji wa azimio hilo: