Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia waathirika wa mafuriko nchini Sri Lanka

IOM yasaidia waathirika wa mafuriko nchini Sri Lanka

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limeanza kutoa msaada kwa waathirika wa mvua kubwa, upepo mkali na maporomoko ya udongo yaliyokumba Sri Lanka wakati wa msimu huu wa sikukuu.

Habari zinasema watu zaidi ya Laki Tatu kwenye wilaya 20 nchini humo wameathirika na hali hiyo ambapo eneo lililoathirika zaidi ni wilaya ya Batticoloa, kwenye jimbo la Mashariki lenye zaidi ya watu Laki Mbili.

IOM inasambaza vifaa kama vile vyandarua, mikeka na vitambaa vigumu kwa visivyoingiza maji kwa ajili ya kufunika vifaa au Kanvasi, msaada ambao unafuatia ombi la serikali ya Sri Lanka.