Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati

Ban alaani mashambulizi kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani vikali mashambulzi yaliyoendeshwa kwenye miji kadhaa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati na kundi la waasi la SELEKA.

Ban amesema kuwa vitendo kama hivyo huwa vinahujumu makubaliano na jitihada za jamii ya kimataifa za kuleta amani chini humo. Amesema kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kulisaidia taifa hilo kukabiliana na changamoto za kutafuta amani. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)