Vurugu Jamhuri ya Afrika ya Kati: UM wahamisha kwa muda baadhi ya wafanyakazi wake

27 Disemba 2012

Umoja wa Mataifa unahamisha kwa muda wafanyakazi wake wasio wa lazika kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na kuzorota kwa usalama na kutotekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, licha ya waasi wa kikundi kiitwacho SELEKA kudai kuwa watasitisha na kuacha kusonga kuelekea mji mkuu Bangui.

Taarifa kutoka ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa utata wa ujumbe kutoka kwa waasi hao na kitendo cha kuendeleza mapigano pengine kinaonyesha nia yao ya kuteka mji huo mkuu.

Hata hivyo uamuzi wa muda wa kuhamisha wafanyakazi hao wa Umoja wa Mataifa hautakwamisha jitihada za chombo hicho za kutafuta amani nchini humo.

Wakati huo huo, kadri hali ya usalama inavyozidi kuzorota, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Margaret Vogt ameendelea kuwasiliana na serikali na viongozi wa waasi kuhakikisha mapigano yanasitishwa na kuanzisha mashauriano kama ilivyopendekezwa na jumuiya ya uchmi ya nchi za Afrika ya Kati tarehe 21 mwezi huu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter