Hali ya usalama huko Goma, watu mashuhuri watoa ombi kwa UM

26 Disemba 2012

Kundi la watu mashuhuri, wakiwemo Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac na Balozi wa mfuko wa Danielle Mitterrand, Valérie Trierweiler ambaye pia ni rafiki wa rais wa sasa wa Ufaransa, wametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kupitisha azimio litakaloruhusu askari wa kulinda amani wa Umoja huo huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, MONUSCO kuongezewa mamlaka ya kutekeleza wajibu wao nchini humo.

Katika ombi lao maalum lililochapishwa kwenye gazeti la kifaransa “Le Monde”, kundi hilo limesema ukatili nchini DRC umefikia kiwango kipya ambapo tayari watu 25 wametia saini ombi hilo akiwemo bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali.

Watu hao waliotia saini wanadai kuwa waasi wa kikundi cha M23 wakiwa na sare madhubuti wanarandaranda mjini Goma wakipandikiza mbegu za chuki huku wakifanya mauaji.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter