UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Syria

26 Disemba 2012

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamadunia, UNESCO, Irina Bokova amelaani mauaji ya mwandishi wa habari wa televisheni nchini Syria, Haidar al-Sumudi .

Bi. Bokova amesema amesikitishwa na mauaji ya mwandishi huyo pamoja na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya waandishi wa habari nchini Syria na kusema uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi ya kila mtu. Amesema hakuna jambo lolote linaloweza kuhalalisha ukandamizaji wa haki hiyo, hivyo ametaka pande zote zinazozozana nchini humo kutambua hadi ya waandishi wa habari na kuwaacha wafanye kazi yao.

Haidar al Samudi aliuawa tarehe 22 mwezi h nje ya nyumba yake kwenye mji mkuu wa Syria, Damascus na kufanya idadi ya waandishi wa habari waliouawa nchini humo mwaka huu pekee kufikia 41.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter