Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la UM lakamilisha sehemu kubwa ya kikao chake cha 67

Baraza Kuu la UM lakamilisha sehemu kubwa ya kikao chake cha 67

Kufuatia mazungumzo ya siku kadhaa, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekalimisha sehemu kubwa ya kikao chake cha 67 kwa kupitishwa kwa azimio mbili kutoka kwa kamati za usimamizi na bajeti.

Baraza hilo lenye wanachama 193 limechukua maamuzi kutokana na jinsi vile wanachama watakavyoweza kuchangia bajeti za shughuli za kulinda amani kwa muda wa miaka mitatu ijayo, pamoja na bajeti ya mwaka 2013 iliyopendekezwa ya masuala ya kisiasa. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)