Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baridi yashika kasi Syria, wakimbizi wa ndani hali zao taabani

Baridi yashika kasi Syria, wakimbizi wa ndani hali zao taabani

Ikiwa imepita kiasi cha siku 650 tangu kuanza kwa machafuko nchini Syria, idadi kubwa ya watu sasa wameingia kwenye wakati mgumu wa kusaka hali ya joto katika wakati ambapo kiwango cha nyuzi joto kikishuhudiwa kupungua.

Kiwango hicho cha nyuzi joto kinatazamiwa kushuka zaidi kuanzia mwezi ujao ambao taifa hilo linakumbwa na hali mbaya zaidi ya baridi.

Mwakilishi wa shirika la utoaji wa huduma za usamaria mwema nchini humo Radhouane Nouicer amesema kuwa kushika kasi kwa msimu wa baridi kali kunaacha maswali mengi juu ya ustawi wa jumla wa wananchi wa eneo hilo walio katika kambi za muda. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)