Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kuwarejesha makwao raia wa Sudan Kusini walio hatarini Sudan waendelea leo: IOM

Mpango wa kuwarejesha makwao raia wa Sudan Kusini walio hatarini Sudan waendelea leo: IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la wahamiaji, IOM hii leo limeanza tena mpango wa kuwarejesha makwao raia wa Sudan Kusini kutoka mjini Khartoum ambao maisha yao yako hatarini.

IOM imesema raia hao wanaorejeshwa kwa ndege ni pamoja na wazee, wagonjwa na wengineo na mpango huo umeanza tena leo baada ya kusitishwa kufuatia kuanguka kwa ndege mwezi Novemba. Afisa wa IOM, Filiz Demir amesema zoezi hilo linalohusisha raia 300 litaendelea hadi Alhamisi. Jason Nyakundi anatupa taarifa zaidi:

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)