Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgao mkubwa zaidi wa mahitaji muhimu waendelea huko Goma, DRC: IOM

Mgao mkubwa zaidi wa mahitaji muhimu waendelea huko Goma, DRC: IOM

Mamia ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wamekosa makwao kutokana na machafuko yanayojiri katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo wameanza kupokea misaada muhimu ikiwemo vifaa vya kujikimu huku wasambazaji wa huduma hizo wakikabiliana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Kiasi cha familia 23,000 zilizoko jimbo la Kaskazini ya Kivu, kimepatiwa vifaa vya dharura ikiwa ni kiwango kikubwa cha misaada kusambazwa katika eneo hilo kwa mwaka huu.

Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF Barbara Bentein amesema kuwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha eneo la Goma, zinatia hali ya wasiwasi kwa watoto ambao hunyeshewa na mvua hizo lakini hukosa nguo za kunadilisha. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)