Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake, ikiwemo ukatili, kwa madai eti ni utekelezaji wa mila na desturi za jamii husika. Mathalani ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike, vipigo, uminyaji wa matiti ya watoto wa kike kama madai ya kumlinda mtoto dhidi ya kutumbukia kwenye ngono mapema na kadhalika.

Moja mwa njia muafaka za kupambana na unyanyasaji huo dhidi ya kinamama ni kuhamasisha vyombo vya usalama ili navyo vikipata taarifa za watuhumiwa viweze kufanya uchunguzi na sheria ichukue mkondo wake.

Kwa dhamira hiyo, mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu jukumu la vyombo vya usalama katika kutokomeza maovu dhidi ya wanawake na wasichana ulifanyika wiki hii mjini Bujumbura, nchini Burundi. Mkutano huo ulioandalia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kinamama UN Women ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka mataifa 33 ya Afrika.

Moja mwa maazimio ya mkutano huo ni kubuni taasisi za ushirikiano kati ya raia na polisi ili kufichua maovu hayo na kuanzisha vituo vya kuwapokea wahanga wa maovu ya kijinsia.

Ungana na mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA aliyeshiriki mkutano huu na kutuandalia makala haya.