Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha hatua ya Senegal ya kumfungulia mashtaka rais wa zamani wa chad Habre

UM wakaribisha hatua ya Senegal ya kumfungulia mashtaka rais wa zamani wa chad Habre

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha hatua ya bunge la Senegal ya kupitisha sheria ya kubuniwa kwa sehemu ya mahakama itakayoendesha kesi dhidi ya rais wa zamani wa Chad Hissene Habre.

Ofisi hiyo inasema kuwa imekuwa ikiunga mkono jitihada za Muungano wa Afrika AU za kuhakikisha kuwepo uwajibikaji kufuatia ukiukaji wa haki za binadamu ulioshuhudiwa wakati wa utawala wa rais Habre. Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa maiaka 70 amekuwa kwenye kifungo cha nyumbani tangu mwaka 2005 nchini Senegal alikokimbilia baada ya kupinduliwa mwaka 1990. Hata hivyo amekanusha madai ya kuwaua na kuwatesa maelfu ya wapinzani wake.